Stori za Mastaa

YOUNG KILLER AMALIZANA NA JOH MAKINI BAADA YA KUSEMA HAYA…

Jan 18, 2017 GongaMx

Young Killer ana mabadiliko kwenye moyo wake. Licha ya mstari wake controversial kwenye ngoma yake mpya, Sinaga Swaga, unaopigilia msumari maoni ya baadhi ya watu kuwa Joh Makini anabebwa, rapper huyo amedai kuwa Mwamba wa Kaskazini hakosi kwenye top 3 yake ya wachanaji bora wa Bongo.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, rapper huyo amedai kuwa si sahihi watu kusema kuwa Joh Makini anabebwa na hivyo kukinzana na mstari wake kwenye Sinaga Swagga.

“Joh ni brother ambaye anafanya kazi zake nzuri, sidhani kama angekuwa anaimba ‘maua madogo yapendeza’, angekuwa anaimba nyimbo zile halafu tunaona anashine, tungekuwa tunaona sio sawa, lakini kwakuwa anaimba ngoma ambazo tunaona zinaeleweka naona ni kauli ambayo sio nzuri.”

Mtangazaji wa show hiyo, Dullah alimchallenge kwa kigongo cha swali jingine kuwa kama amesema hivyo iweje akubaliane na maneno mtaani kuwa Joh anabebwa na rapper huyo kujibu, “ni kwasababu lisemwalo lipo kama halipo linakuja, ndio wengi wanavyosema, kwanini kila mtu anasema hilo suala?”

Anachokifanya Young Killer ni kile wazungu wanakiita Damage Control!

Comments

comments