News

WCB KUWAPA NYUMBA TANO WAATHIRIKA WA MAFURIKO IRINGA

Dec 13, 2016 GongaMx

Lebo ya WCB imeahidi kutoa nyumba tano kwa ajili ya wahanga wa mafuriko mkoani Iringa kati ya 85 zilizoharibika.

Diamond Platnumz ambaye ni bosi wa lebo hiyo amemuahidi Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela aliyetembelea kwenye ofisi za WCB kuwa watachangia nyumba hizo na kuzikabidhi siku ya sikukuu ya Christmas watakapokuwa wakitumbuiza mkoani humo.

Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameandika:

Tunakushkuru sana Mkuu wa wilaya Iringa Mh: Richard Kasesela kwa Kututembelea Vijana wako na pia kutukaribisha rasmi Iringa kuja kula Sikukuu ya X-mass tareh 25/12 /2016 kwenye #VodacomWasafiFestival …lakini pia nitumie fursa hii kuwapa pole ndugu zetu wa IRINGA kwa kubomokewa ama kupoteza makazi zaidi ya 86 kutokana na Mafuriko yaliyotokea….kwakuamini kuwa sisi sote ni binaadam na kuwa la kwako ni sawa na la kwangu, tukiwa kama @Wcb_Wasafi tumeahidi kutoa Nyumba Tano kwajili ya wahanga hao na Panapo Majaaliwa tutazikabidhi Nyumba hizo siku tutayofika Iringa🙏….. ndugu zetu wapendwa kwa alie na chochote pia anaweza kuwachangia ndugu zetu wa Iringa, waweze fanikisha makazi ama Nyumba hizo 85….

Comments

comments