Fashion Lifestyle News Uncategorized

i-TIP | Tambua uvaaji wa “BANGILI aka BRACELET”

Jun 25, 2016 frank

iTIP ni sehemu ya GongaMX ambayo itakuwa inakuhabarisha na kukushauri nini unatakiwa kufanya katika mambo mbali mbali ya uvaaji wa kila aina ya mavazi ambayo tunayatumia katika maisha yetu ya kila siku. iTIP itakuwa inakupa “Tips” za jinsi ya utumiaji wa mavazi kwa wakati na nyakati kuweza kukusaidia kufanya maamuzi mazuri katika uvaaji wako kuanzia Nguo, Miwani, Pochi, Viatu, Saa za mkononi, Nguo za ndani na chochote kile ambacho unakifikilia wewe ambacho unakivaa katika maisha yako ya kila siku.

BANGILI aka BRACELET: Ni muhimu sana kuzingatia rangi na aina ya uvaaji wa BANGILI (BRACELET) kutokana na muonekano wa nguo unayovaa kwa muda huo. Inapendeza sana kama rangi ya ngozi yako, bangili na nguo uliyovaa kutopishana sana kwa kukupatia muonekano wa ajabu wenye rangi nyingi tofauti na kuweza kuharibu muonekano wako.

IMG_20160624_101517

Kwa mfano mtu mweusi anaweza akavalia bangili ya rangi nyeupe, nyekundu, njano n.k au katika mchanganyiko wa rangi zote hizo. Hii kwa kiasi kikubwa inasaidia kuamsha muonekano wake zaidi na wenye kuvutia kwa kuendana na rangi ya mpangilia wake.

IMG_20160624_101458

KUMBUKA: Kuna msemo usemao, UPITAPO MAHALI NA UKAONA WATU WANAKUANGALIA SANA LAZIMA UTAMBUE KUWA, INAWEZEKANA UMEPENDEZA SANA AU UMEHARIBU SANA.

BY: Barrish Hollic

Comments

comments