Fashion Lifestyle Uncategorized

i-Tip | Sanaa ya Mikoba ya Asili

Jul 02, 2016 GongaMx

MIKOBA YA ASILI

Leo ngoja nikupe ‘Tip’ kuhusina na sanaa ya mikoba ya Asili. Kwa hakika tunapo zungumzia urembo katika muonekano wa mikoba ya asili tunakuwa tunamaanisha vitu vingi vinavyo pelekea kukusanya pamoja muonekano wa kuvutia wenye kuacha maswali mengi sana katika macho ya wanao kutazama katika urembo wako.

Kenyan Designer, Adeledejak, Bags Bags, African Design, African Bags

Mikoba toka kwa Kenyan Designer, Adeledejak | African Bags

Muonekano wa mkoba wa asili una nafasi kubwa ya kukupa uhuru katika kukamilisha sehemu ya urembo wako kutokana na aina ya vazi utakalolivaa kwa muda huo.

Hii ni kutokana na jinsi aina hii ya mikoba inavyotengenezwa kwa kuwekwa mpangilio wa rangi zenye kuvutia, rangi tulivu zisizo kuwa na mchanganyiko wa muonekano mkali kuweza kupoteza muonekano wa vitu vingine ulivyovaa na pia aina ya mali ghafi zilizotumika kutengenezea mkoba huo (materials) n.k….

Ghanaian designer Akosua Afriyie-Kumi is one of the hottest names in African fashion.

Ghanaian designer Akosua Afriyie-Kumi mmoja wa designers wakubwa sana kwenye African fashion.

Kwa asilimia kubwa aina hii ya mikoba hupendelewa sana kutumiwa na wanawake, hii ni kwa sababu muundo wake, muonekano na nakshi za urembo zinazotumika katika kutengenezea hazimruhusu mwanaume kutumia kama sehemu ya muonekano wake.

Pia katika ukuaji na kuendelea kwa fashion ya mikoba hii, sasa hivi imekuwa ikionekana katika mionekano wa tofauti yenye kuvutia mara dufu zaidi na kuweza kufanya muongezeko wa ubunifu kwa kuweza kuwepo na style mpya tofauti mara kwa mara kutokana na nyakati.

IMG_20160702_121232 IMG_20160702_121217

Kwa mwanamke unaependelea sana kubeba aina hii ya mikoba kwa ajili ya kukamilisha urembo wako, basi unaweza ukavalia mavazi ya aina yoyote yale iwe jeans, suit, dira na hijab, kitenge, khanga n.k na bado utaonekana ni mwenye kupendeza, kuvutia na mwenye kwenda na fashion.

755f9b430572fa422a7dacd706b8f87f

“Mwanamke,  jiangalie sana kwenye kioo kuweza kuona mchanganyiko unaouvaa kabla ya kutoka, ndio maana ya kuwa na kioo ambacho unakuwa na uwezo wa kujiona mwili mzima ndani ya nyumba ni muhimu sana.” 

BY: Barrish Hollic

Comments

comments