Stori za Mastaa

NAY WA MITEGO ADAI MAHABA MAZITO ANAYOPEWA NDIYO YAMEMPELEKEA KUANDIKA NGOMA YA ‘SIJIWEZI’

Dec 19, 2016 GongaMx

Msanii wa muziki wa hip hip Nay wa Mitego amedai hawezi kuandika wimbo wa mapenzi kama hana feeling ya mapenzi au hayupo kwenye mahusiano.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Nay amedai wimbo wake mpya ‘Sijiwezi’ ameuandika kutokana na kupewa mahaba mazito kutoka kwa mpenzi wake.

“Mimi siwezi kuandika wimbo wa mapenzi bila kupata feeling ya mpenzi kutoka kwa mpenzi wangu au watu wangu wa karibu ndio maana hata unaona na nyimbo chache sana za mapenzi,” alisema Nay. “Hata Sijiwezi umetokana na maisha yangu ya ndani na mpenzi wangu. Nikaona hapa kuna sababu ya kuandika kitu na kweli nimefanya na namshukuru Mungu ngoma inaenda,”

Rapa huyo anawashukuru mashabiki wa muziki wake kwa kuupokea vizuri wimbo huo katika kipindi cha muda mfupi.

Comments

comments