News

“NAJIVUNIA KUUTANGAZA MUZIKI WA HIP HOP KIMATAIFA KWA MWAKA 2016” -JOH MAKINI

Dec 15, 2016 GongaMx

Msanii wa hip hop wa Kundi la Weusi, Joh Makini amefunguka na kuzungumzia mafanikio ya muziki wake ndani ya mwaka 2016 ambao unaenda ukingoni kumalizika.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Joh amedai licha ya mafanikio yake binafsi lakini anafurahi jinsi alivyoplay part yake katika kuutangaza muziki wa hip hop kimataifa.

“2016 umekuwa ni mwaka mzuri sana kwangu na kwa muziki wangu kiujumla kwa sababu nimeweza kufanya vitu vingi vikubwa kitaifa na kimataifa na project mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine nimeendelea kuutanua muziki wa hip hop nje ya Tanzania,” alisema Joh “Kwa hiyo nashukuru Mungu na pia nawashukuru wote ambao walikuwa nyuma yangu kwa namna yoyote katika kutoa support kwa Joh Makini,”

Joh Makini ndani ya mwaka huu amefanya vizuri zaidi na wimbo kama Don Bother akiwa amemshirikisha AKA wa Afrika Kusini pamoja na Perfect Combo akiwa amemshirikisha Chidinma wa Nigeria.

Comments

comments