Stori za Mastaa

NAHREEL AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZA KUIZUA NGOMA YA JOH MAKINI NA DAVIDO

Dec 21, 2016 GongaMx

Mwanamuziki na mtayarishaji wa muziki kutoka studio za ‘The Industry Studio’ Nahreel amefunguka na kusema yeye hajazuia ngoma ya Joh Makini pamoja na Davido kwani hana sababu ya kufanya hivyo na kusema anaamini kuwa wimbo huo utatoka muda si mrefu.

Nahreel alisema hayo kupitia kipindi cha eNewz na kusema anadhani tayari Joh Makini huenda akawa ameshafanya hadi video ya ngoma hiyo kipindi cha karibuni ambapo alikwenda Afrika ya Kusini.

“Hizi mambo ya kuwa nimezuia ngoma ya Joh Makini na Davido umeitoa wapi? Hii ngoma hatujazuia kwanini nizuie ngoma ya Joh na Davido? Hii ngoma inaenda kutoka na Joh Makini nadhani amesha shoot video manake alienda South Afrika juzi juzi hapa wamesha shoot kwa hiyo stay tune inakwenda kutoka”.

Kwa upande wake Joh Makini katika moja ya mahojiano alisikika akisema kuwa mwakani kutakuwa na ngoma nyingi sana bora kutoka kwa Weusi na si bora kazi ila kazi nyingi bora.

Comments

comments