Fashion

MUSTAFA HASSANALI AJINASIBU KUJA NA UBUNIFU MPYA WA MAVAZI MWAKA HUU

Aug 05, 2016 GongaMx

Mbunifu mahiri wa mavazi nchini, Mustafa Hassanali amewaahidi makubwa wadau wake wa mavazi na tasnia nzima kwa ujumla kuwa anakuja na aina mpya ya kazi zake za kibunifu katika fani hiyo.

Hassanali ambaye anatamba katika fani hiyo akiwa na onesho lake la Swahili Fashion ambalo ni onesho kubwa zaidi la mavazi Afrika Mashariki na Kati alisema kuwa bado fursa zipo nyingi katika fani hiyo.

Alisema kuwa katika kuendelea kuwakilisha vyema Tanzania ndani na nje ya nchi kwenye tasnia ya mitindo anaendelea kujipanga zaidi hasa katika kubuni mavazi ya aina mbalimbali ya kiume na ya kike.

Alisema kuwa katika onesho lake la mavazi aliloshiriki kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya huduma za Shirika la Ndege la Afrika Kusini lililofanyika Capetown, Afrika Kusini alionesha baadhi ya kazi zake za mwaka huu.

Alisema kuwa katika onesho hili alionesha mavazi ya kiume ambapo alisema kuwa ilikuwa ni sehemu kubwa ya kuendelea kutangaza kazi zake nje ya nchi.

Alisema kuwa Afrika Kusini imekuwa moja kati ya nchi ambazo amekuwa akishiriki mara kwa mara kuonesha kazi zake za kibunifu na amekuwa na soko pia.

“Huu mwaka ni moja kati ya miaka ambayo ninaona kuwa kuna mengi ya kufanya katika tasnia hii na hasa ikizingatiwa kuwa kuna kazi za ndani na nje ya nchi na zote ni muhimu kwangu na kwa tasnia nzima,” alisema. Mustapha ameshafanya kazi katika majiji 31 na nchi 21 hadi sasa akiwa kama mbunifu wa mavazi kutoka Tanzania.

Comments

comments