News

“MATATIZO YA KIFAMILIA YAMESHINDWA KUMRUDISHA 20% KWENYE MUZIKI 2016” -MAN WALTER

Dec 21, 2016 GongaMx

Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva kutoka ‘Combination Sound’,  Man Water amefunguka na kuweka sawa sababu ambazo zimefanya msanii wake 20% kushindwa kurudi kwenye muziki mwaka 2016 licha ya kuachia kazi moja.

Man Water kwenye kipindi cha eNewz alidai sababu kubwa ambayo imepelekea msanii 20% kushindwa kurudi kama ambavyo watu walikuwa wakitarajia baada ya msanii huyo kupata ‘Management’ ambayo ipo chini yake ni kutokana na kushindwa kutimiza mipango yao kutokana na matatizo ya kifamilia ambayo 20% alikuwa akikabiliana nayo lakini pia mipango yao haikuwa mizuri jambo ambalo hawataki litokee tena.

“Kwanza kabisaa mipango ambayo tulikuwa tumepanga ilishindwa kutimia, tulikuwa na mipango ya kufanya video na tunaangalia video ingekuaje, bajeti ipoje yaani kulikuwa na mambo mengi sana wakati huo huo 20% alifiwa na dada yake, mimi mwenyewe nikafiwa, yaani kulikuwa na mambo mengi sana hivyo kuahirisha kukawa kwingi sana. Unakuta upande mmoja kukiwa sawa kwingine kuna kuwa siyo, hivyo muda huu tunaomba Mungu mengine yasitokee yale ya dharura ili katika hii new page tujue tunafanya nini, lakini 20% ana stock hapa na studio kuna nyimbo kama tano” alisema Man Water

Comments

comments