Adverts News

JIDE AIPELEKA ‘NAAMKA TENA TOUR’ TANGA, GEITA NA MWANZA. TAREHE HUSIKA HIZI HAPA..

Aug 22, 2016 GongaMx

Ile ziara ya mwanamuziki Lady Jaydee ya “Naamka Tena Tour” inaendelea tena ambapo safari hii ni zamu ya mikoa Geita, Mwanza na Tanga.

Ziara itaanza Agosti 26 jijini Tanga ambapo Lady Jaydee atakuwa Live katika ukumbi wa Tanga City Lounge kwa kiingilio cha sh 10000/= tu huku ziara hiyo ikiendelea Septemba 2 kwa Jide kujumuika na bendi yake Mkoani Geita katika ukumbi wa Ambassador huku viingilio vikiwa ni sh 20000 kwa VIP na 10000 kwa kawaida.

Ziara hiyo itaendelea Septemba 3 jijini Mwanza ambapo Jide atakuwa pamoja na bendi yake kwenye ukumbi wa Villa Park Resort kwa kiingilio cha Sh 50000/= kwa VIP na sh 10000 kwa siti za kawaida lakini utalipia 20000 siti za kawaida kama ukinunulia tiketi getini.

13715159_1040017839439567_797046862_n

Comments

comments