Uncategorized

HIZI NDIZO BEI ZA VIINGILIO EATV AWARDS MLIMANI CITY DESEMBA 10

Dec 06, 2016 GongaMx

East Africa Television Ltd imeweka wazi viwango vya viingilio kwa ajili ya kushuhudia tukio kubwa na la kihistoria litakalosimamisha tasnia ya burudani nchini, la EATV AWARDS.

Tukio hilo ambalo linatarajiwa kufanyika siku ya tarehe 10 Desemba 2016 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambalo ni la kwanza kwenye historia ya burudani nchini, litakuwa na viingilio vya kawaida ambavyo kila mtanzania ataweza kumudu gharama zake, na kushuhudia historia ikiandikwa.

Kwa tiketi za VIP zitapatikana kwa shilingi elfu 50, huku zile za kawaida zitapatikana kwa shilingi elfu 20, na iwapo mtu atanunua kwa M-PESA, tiketi za VIP atanunua kwa shilingi 45, 000 na kawaida akinunua kwa shilingi 18,000.

Tiketi hizo zitapatikana, Samaki Samaki City Centre, Masaki na Mlimani City, Namanga Best bite na studio za East Africa TV na Radio.

Sherehe hizo zitahudhuriwa na watu mbalimbali maarufu kutoka ndani na nje ya nchi, huku wengine wakiwa ni ‘suprise’ kwa wadau na mashabiki watakaofika, huku jukwaa likisimamiwa na mkali wa MIC kabla hajazaliwa , Salama Jabir.

Comments

comments