News

HIKI NDICHO ALICHOSEMA ALI KIBA KUHUSU KUTOA NGOMA NYINGINE KWA SASA

Dec 14, 2016 GongaMx

Mshindi wa tuzo tatu za EATV, Alikiba amedai hawezi kuachia nyimbo mfululizo wakati bado kuna nyimbo zake ambazo bado zinafanya vizuri.

Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo Aje, amedai kuachia wimbo mpya wakati kuna nyimbo bado zinafanya vizuri ni kujitia hasara.

“Naamini mimi muziki wangu una thamani kubwa sana ndio maana nyimbo zangu zinakaa muda mrefu sokoni,”Alikiba aliwaambia waandishi. “Kwahiyo bidhaa yangu inavyokaa muda mrefu sokoni siwezi kuleta bidhaa nyingine kwa sababu hii ya kwanza haijaisha, nataka watu wapate watosheke ili wakiridhika niweze kutoa nyingine kwa sababu nitapata hasara kama nitatoa bidhaa nyingine ambayo itakuwa nzuri kuliko ile ambayo ipo sokoni.,”

Pia muimbaji huyo amesema remix ya wimbo ‘Aje’ ipo tayari ila kwa sasa hawezi kuitoa kwa kuwa anazipa muda kazi ambazo zimetoka akiwa ameshirikiana na wasanii wenzake.

Comments

comments