News

CPWAA AIFUFUA UPYA LEBO YAKE YA BRAINSTORM; ATHIBITISHA KUENDELEA KUWASIMAMIA ‘WADANANDA’

Dec 16, 2016 GongaMx

Baada ya kimya cha muda mrefu, Cpwaa ameifufua lebo yake ya muziki, Brainstorm Music

Rapper huyo aliiambia 255 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa bado lebo yake inawasimamia Wadananda.

“Tayari nimeshasaini Wadananda, bado kuna vijana wengi wanahitaji msaada, Mungu atusaidie tupate pesa tuweze kuwasaidia. Sometimes sio pesa tu hata muongozo unatosha kwahiyo Mungu aendelee kutupa hekima na busara. Kwa hiyo I ‘ll sign more artist na kuna wengi ambao mpaka sasa hivi sitaki kuwataja majina lakini mchango wangu upo mkubwa,” amesema.

“Walipokwama wanahitaji connections mimi nimewasaidia, wanahitaji media connection nimewasaidia, wanahitaji ideas nimesaidia, yaani vitu vingi kwahiyo bado ni kitu ambacho nitaendela kukifanya mpaka siku naingia kaburini,” ameongeza.

Comments

comments