News

BARAKA THE PRINCE AMSAJILI LORD EYEZ KWENYE LEBO YAKE MPYA YA BANA

Dec 13, 2016 GongaMx

Rapper mkongwe wa Nako 2 Nako na aliyekuwa mmoja wa members wa kundi la Weusi, Lord Eyez atakuwa chini ya usimamizi wa label mpya mjini – BANA, inayomilikuwa na Barakah The Prince.

Barakah ameitangaza label yake hiyo Jumanne hii wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa TV. Muimbaji huyo wa Nisamehe amedai kuwa Lord Eyez ataungana na mpenzi wake, Naj kama wasanii wa label hiyo na kwamba hivi karibuni nyimbo zao zitatoka.

Amedai kuwa lengo la kumchukua Lord Eyez ni kutokana na kukubali uwezo wake na kwamba kutokana na kutumbuiza naye kwenye show kadhaa, amegundua kuwa ana mashabiki kibao.

Comments

comments