News

BAADA YA BONTA KUUPONDA USAJILI WA LORD EYEZ KWA BARAKA THE PRINCE, JOH MAKINI NAYE ATOA NENO

Dec 20, 2016 GongaMx

Hatimaye Joh Makini amezungumza kuhusiana na taarifa za Lord Eyez kusainishwa kwenye label ambayo Barakah The Prince ameianzisha.

Joh amesema pamoja na kuwa Lord Eyez ni mshkaji wake mkubwa, ana uhuru wa kuchukua uamuzi anaodhani una manufaa kwake.

“Mimi Lord Eyez mbali na muziki ni mshkaji wangu sana, we are family. Hata ninavyoongea na wewe wiki moja nyuma kabla sijaenda South Africa tulikuwa wote usiku huo,” amesema Joh. “Mwisho wa siku unajua naheshimu sana maamuzi ya mtu binafsi na sipendi kuingilia. Kwa mfano siwezi kuongelea uamuzi wa yeye kusainiwa au kutosainiwa na Barakah The Prince sababu that’s him,” ameongeza.

“Naheshimu kila kitu ambacho yeye anakifanya kwasababu mwisho wa siku kila mtu ana njia yake, ana maisha yake, kila mtu ana maamuzi yake. Unajua huwezi kumuamlia mtu mzima.”

Comments

comments