News

ALICHOKISEMA LADY JAYDEE KUHUSU MFUMUKO WA WASANII KUMILIKI LEBO ZA MUZIKI HIKI HAPA…

Dec 08, 2016 GongaMx

Msanii mkongwe wa muziki Lady Jay Dee amesema hana mpango wa kuanzisha record label kwa kuwa kuna baadhi ya wasanii wanafanya hivyo

Alisema hayo wiki hii wakati alipowatembele wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Kampasi ya Mlimani) na kuzungumza nao mambo mbalimbali kuhusu muziki.

Muimbaji huyo alisema wasanii wengi wanaanzisha record label kwa kuwa wamewaona wasanii fulani wamefanya hivyo.

“Sio lazima kila mtu awe na record label,” alisema Lady Jay Dee. “Kila msanii ana namna ambavyo anafanya kazi. Kwahiyo suala la record label kwa sababu msanii fulani anayo sio lazima,”

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka wasanii wachanga kuonyesha vipaji vyao kwanza kabla hawajakimbilia kuoamba msaada.

Pia alisema yeye kabla ya kuanza kupata nafasi ya kuonyesha kipaji chake alianza kupiga simu redioni na kuimba live ili kuonyesha ni kitu alichonacho.

Comments

comments